Swali: Mimi ni mtu ambaye si msomi ninayependa kuhudhuria darsa za wanachuoni wakubwa. Kwa mnasaba wa ajali nzito nzito ninanukuu maneno ya wanachuoni kuhusu makundi na khatari ya kuwa vikundi vikundi. Matokeo yake baadhi ya watu na marafiki zangu wananikataza. Je, wana haki ya kufanya hivo au kitendo changu mimi ndio sahihi?

Jibu: Hapana, kitendo chako ni sahihi. Allaah Akujaze kheri. Ukiona mtu anajiunga na makundi makundi au anajigawa; wanawagawa watu makundi, mapote na kadhalika, haya ni maovu. Kataza kiasi na uwezo wako na jinsi unavojua. Ni mwenye kupewa ujira kwa hilo – Allaah Akitaka.

  • Mhusika: Imam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´alaal-Hawaa’ 1435-11-22 Referens: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=147367
  • Imechapishwa: 19/04/2015