Swali: Inaweza kutokea niko mahala ambapo kuna watu wengine walioathirika na baadhi ya walinganizi wapotevu ambao wanachuoni wamewatahadharisha. Je, nieleze waliosema wanachuoni kuhusu wao au bora zaidi ninyamaze na khaswa ikiwa walioko kwenye kikao hicho ni watu ´Awwaam?

Jibu: Hapana, usinyamaze. Ukinyamaza ina maana unakubaliana na wao na hivyo ´Awwaam wataona kuwa ni sawa. Bainisha kwa hekima na maneno mazuri. Ikiwa unaweza kuwabainishia suala hilo faragha, fanya hivo. Wakijirudi himdi zote ni za Allaah. Na wasipofanya hivo baada ya hapo wabainishie watu.

  • Mhusika: Imam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tatwhiyr-il-I´tiqaad (1) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13132
  • Imechapishwa: 19/04/2015