Kufumba macho wakati wa kusomewa Ruqyah

Swali: Kuna mji wetu kuna njia wanayoitumia baadhi ya wasomaji Ruqyah. Wanapotaka kumsomea mtu aliyepatwa na kijicho wanamwambia afumbe macho yake na halafu wanamsomea juz katika Qur-aan kisha wanamuuliza alichoona. Mtu yule msomewaji anasema kuwa amemuona fulani bin fulani. Msomaji anamtuhumu ya kwamba huyo ndiye aliyekufanyia uchawi huu au maneno mfano wa hayo. Je, njia hii inajuzu na unawanasihi vijana kujishughulisha na Ruqyah?

Jibu: Ninaamini kuwa njia kama hii ni ya uchawi na ya ki-Shaytwaan. Uislamu umetakasika nayo. Ruqyah ya Kishari´ah iliyofunza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio ambayo Muislamu anatakiwa kutumia. Ama kuhusu njia hii naamini kuwa haikufunzwa na Qur-aan. Kufumba macho na kuona mtu kisha baada ya hapo anatoa hukumu ya kwamba yeye ndiye amemfanyia uchawi. Hii ni natija ya uchawi anayoificha huyu Dajjaal. Kutokana na natija ya uchawi wake ndio anaona mambo kama haya. Allaah ndiye Anajua zaidi ni watu gani anaowaona ambao pengine huyu muonaji akawa anawadhulumu. Inawezekana huyu anayemuona amejitenga mbali kabisa na uchawi. Hii sio dalili ya kwamba huyu ndiye amemfanyia uchawi.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofanyiwa uchawi na yeye akawa anasoma Qur-aan hakumjua aliyemfanyia uchawi mpaka baada ya kuja Jibriyl (´alayhis-Salaam) na kumjulisha mtu huyo na kumwambia ni wapi unapopatikana uchawi huu. Hili ni jambo lisilojulikana kamwe isipokuwa kwa njia ya Wahyi au kwa njia ya mashaytwaan. Huyu aliyemuona sio mtu huyo bali ni Shaytwaan aliyejifananisha na sura ya mtu huyo. Ninavyoonelea hii ni dalili tosha inayoonesha huyu Dajjaal anayejionyesha kwa watu ya kwamba anasoma kwa kutumia Qur-aan ya kuwa ni mchawi na ni Dajjaal na anashirikiana na mashaytwaan. Haijuzu kwa yeyote kwenda kwa mtu kama huyu kama jinsi haijuzu kwa yeyote kumsadikisha kwa mashaytwaan anaowaona na huku anafikiria kuwa ni watu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12067
  • Imechapishwa: 19/04/2015