Swali: Nilifunga siku ya ´Arafah iliyoanguka siku ya Ijumaa bila ya kufunga Alkhamisi kabla yake. Je, nilifanya dhambi?

Jibu: Ninataraji kuwa huna dhambi. Kwa sababu hukukusudia kufunga siku hiyo, ulifunga kwa sababu ni siku ya ´Arafah. Lakini lililo salama zaidi ni kufunga Alkhamisi kabla yake kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataza kwa mwenye kufunga [Swawm ya] Sunnah kufunga siku ya Ijumaa peke yake. Kama tulivyosema ni salama zaidi kufunga Alkhamisi kabla yake hata kama unakusudia kufunga siku ya ´Arafah tu. Hata hivyo ni salama kwa muumini kutilia nguvu na kuafikiana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kujisalimisha na maamrisho yake. Pamoja na hivyo haijuzu kufunga siku ya Ijumaa peke yake kutokana na fadhila zake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza. Lakini hata hivyo ninataraji kuwa mtu hafanyi dhambi lau atafunga tu siku ya Ijumaa kwa sababu ´Arafah imeanguka siku hiyo. Ingawa ni bora na salama zaidi kufunga na Alkhamisi kabla yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.binbaz.org.sa/mat/13717
  • Imechapishwa: 19/04/2015