Vipaza sauti nje ya msikiti katika Tarawiyh

Baadhi yao [maimamu] wanazitoa nje sauti zako kwa kisomo ca Qur-aan kwa kutumia kipaza sauti. Matokeo yake wanawashawishi misikiti ilioko pembezoni, kitu ambacho hakijuzu. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

“Ambaye anasoma Qur-aan wakati ambapo watu wanaswali swalah ya sunnah basi haifai kwake kusoma kwa sauti ya juu ambayo itawashughulisha. Kwani hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwatokea Maswahabah zake wakati walipokuwa wanaswali msikitini akasema:

“Enyi watu! Kila mmoja wenu anamnong´oneza Mola wake. Hivyo wamoja wasisome Qur-aan kwa sauti juu ya wengine.”[1]

[1] Tazama ”Majmuu´-ul-Fataawaa (23/61-64))

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/171)
  • Imechapishwa: 06/04/2022