Maimamu wanaokhitimisha Qur-aan kila baada ya siku kumi katika Tarawiyh

Baadhi ya maimamu wa misikiti wanasoma Qur-aan haraka na wanairefusha ili wapate kukamilisha Qur-aan katika lile kumi la mwanzo na la katikati. Anapokamilisha basi  wanaikimbia misikiti yao na wanamweka mtu mwengine na wanasafiri katika ´Umrah ilihali nyuma pengine wamemwacha mtu ambaye hafai kufanywa imamu. Hilo ni kosa kubwa, upungufu mkubwa na kupoteza ile kazi aliyopewa ya kuwaswalisha waswaliji mpaka mwishoni mwa mwezi. Kwani kazi aliyopewa ni lazima kuitekeleza na kufanya ´Umrah ni jambo lililopendekezwa. N vipi ataacha jambo la lazima juu yake kwa ajili ya jambo lililopendekezwa? Kubaki kwake msikitini kwa ajili ya kazi yake ni bora kuliko kufanya ´umrah.

Baadhi ya maimamu wengine wakimaliza Qur-aan basi wanawepesisha swalah na wanapunguza kisomo katika nyusiku zengine za mwezi ambazo watu huachwa huru kutokamana na Moto. Kana kwamba watu hawa wanaona kuwa lengo la Tarawiyh na Tahajjud ni kusoma Qur-aan yote na si kuhuisha nyusiku hizi zilizobarikiwa kwa kusimama kwa ajili ya kumwigiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutafuta fadhilah zake. Huu ni ujinga wao na kucheza na ´ibaadah. Tunataraji kwa Allaah atawarudisha katika usawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/171)
  • Imechapishwa: 06/04/2022