Vinavyookotwa kuwapa jumuiya za misaada na wamasikini

Swali: Inatokea wakati mwingine wateja wanasahau vitu vyao katika duka letu la nguo. Vitu hivyo vinabaki kwetu mwaka mzima na wamiliki wavyo hawaji. Je, baada ya hapo vinakuwa ni vya mmiliki wa duka au tuvipeleke katika jumuiya za misaada?

Jibu: Ni vizuri ikiwa mtavitoa kuwapa jumuiya za misaada. Vilevile haina neno ikiwa mtawapa watu wenye kuhitaji na kunuia thawabu ziwaendee wenye navyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (31)
  • Imechapishwa: 05/03/2022