Vikao vya elimu nyumbani fadhilah zake ni sawa na msikitini?

Swali: Je, watu wanapata fadhilah zilezile[1] endapo watakusanyika katika nyumba za kawaida?

Jibu: Kunatarajiwa kwao – Allaah akitaka. Lakini msikitini ndio bora na kuna manufaa zaidi kwa watu. Wakifanya nyumbani kunatarajiwa kwao kupata kheri hii.

[1] Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyeeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hawatokusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakikisoma Kitabu cha Allaah na wakikidurusu kati yao, isipokuwa wanateremkiwa na utulivu, rehema huwafunika na Malaika huwazunguka na Allaah huwataja kwa wale walioko Kwake.” (Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (1308).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21595/هل-يشمل-البيوت-فضل-مجالس-الذكر
  • Imechapishwa: 27/08/2022