Swali: Hadiyth wakati walipokuja mabedui Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

”Nendeni na mnywe mkojo na maziwa yake.”

Jibu: Hawa ni watu ´Uraniyyuun walipatwa na maradhi ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawatuma wakijitibu kwa mkojo wa ngamia na maziwa yake.

Swali: Wanywe mkojo?

Jibu: Hapana vibaya. Ni msafi kwa kujitibu nao. Kila mnyama ambaye analiwa nyama yake basi mkojo wake ni msafi; mkojo wa ngamia, mkojo wa ng´ombe au mkojo wa mbuzi na kondoo.

Swali: Kwa hiyo hautakiwi kuoshwa?

Jibu: Kwa ajili ya usafi. Ni kwa lengo la usafi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21583/ما-حكم-التداوي-بابوال-الابل-والبانها
  • Imechapishwa: 27/08/2022