Swali: Mimi ni kijana nimepewa mtihani wa kujitoa manii na nimeshindwa kujikwamua nalo, mara hutubia na mara nyingine narejea. Niko katika hali hii kwa miaka mingi. Ni ipi nasaha yako kwangu na vipi naweza kujikwamua nalo? Ninapofanya hivo ni lazima kuoga?

Jibu: Ndio. Huu ni mtindo mchafu. Unaweza kujikwamua nalo na si kama ulivosema. Unaweza kujikwamua nalo kwa kumcha Allaah na kuliacha na kujitenga nalo mbali. Ama ukiendelea kufanya hivo itakuzidia na shaytwaan atakupambia nalo. Ni juu yako kuleta tawbah ya kweli na kujitenga mbali. Miongoni mwa masharti ya tawbah ni kuacha dhambi hiyo. Achana na mtindo huu mchafu na muombe Allaah (´Azza wa Jall) msaada.

Kuhusu kuoga, ukitokwa na manii ni lazima kwako kuoga. Pamoja na kwamba unapata madhambi na ni haramu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (20) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-2-15.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020