Swali: Wengi katika watoto wetu wanaopelekwa kusoma nje ya nchi hukaa pamoja na familia za manaswara kwa hoja kwamba wanajifunza lugha ya kingereza kutoka kwao. Lakini wakati huohuo hula pamoja nao nyama ya nguruwe, hunywa pamoja nao pombe, hufanya uzinifu katika nyumba zao na huacha swalah kwa kujikombakomba na kujipendekeza, kisha hurudi mikono mitupu – hakuna cha swalah – bali ni maadui wa dini na wenye kuupiga Uislamu. Ni upi msimamo wa serikali na wanazuoni wake watukufu kuhusu khatari hii kubwa?
Jibu: Hili linatokea kwa baadhi yao. Kwa sababu hiyo wanazuoni wanatoa nasaha ya kutokutuma wanafunzi nje ya nchi. Serikali pia imeahidi kutowatuma isipokuwa kwa dharurah. Kwa hiyo ni wajibu kutekeleza jambo hili na asiwepo anayesomea nje ya nchi isipokuwa kwa dharurah, katika mambo adimu na ya juu sana ambayo hayakupatikana anayefundisha hapa. Asitumwe isipokuwa yule anayejulikana kuwa na msimamo wa dini, elimu, uongofu na usawa kwa mpangilio maalum. Hawa walioashiriwa na muulizaji ambao wanaoshuka kwa makafiri na kushiriki nao katika vyakula na vinywaji, hawa bila shaka ni khatari kwa waislamu na shari yao ni kubwa. Wakirudi na wakapewa nyadhifa basi madhara yao huwa makubwa bila shaka.
Kwa hiyo ni wajibu kuzuia watu hawa na wasichanganyike na makafiri. Wakisafiri kwa ajili ya kujifunza, basi wawe wakisimamiwa na wawe katika hali ya kutengwa, mbali na kuchanganyika na makafiri. Wajifunze lugha wanayoitaka kwa waalimu, si kwa wanawake, wasichana na wenye kueneza uharibifu ardhini, hapana. Aliyesafiri kwa ajili ya kujifunza achanganyike na waalimu wanaofundisha, achukue elimu kutoka kwao na kutoka kwa wenzake wanaosoma naye, si kwa wanawake majumbani, anamjia mwanamke kwa mapambo yake na utovu wake wa haya na akafanya naye maovu. Hilo ni miongoni mwa mabalaa makubwa. Madhumuni ni kwamba wengi wa hawa wanafunzi – au karibu wote – hupatwa na shari na ufisadi wanapokwenda huko. Ni wachache mno ndio huokoka na kusalimika.
Kwa hiyo ni wajibu kwa watawala, kama walivyowafikishiwa na wanavyofahamu – Allaah awape tawfiyq – mara kwa mara kutokuwatuma wanafunzi nje ya nchi na wasitumwe nje isipokuwa yule ambaye dharurah imesema lazima, katika mambo machache adimu ambayo hayana anayefundisha hapa. Ni lazima pia kutafutwa anayefundisha hapa. Lakini ikilazimu, basi iwe kwa idadi ndogo sana. Aidha wawe watu wanaojulikana kwa wema, uongofu, kheri na akili iliyo sawa. Pamoja na hayo pia wawe wanakaguliwa na watu wa kheri na uadilifu ili huenda wakasalimika au wengi wao wasalimike.
Swali: Je, baba ana wajibu wa kumzuia mwanawe kwenda?
Jibu: Baba ana jukumu la kujitahidi katika hilo. Baba na wasio baba, baba na ndugu wanapaswa kusaidiana katika kuzuia jambo hili na wafanye juhudi zao zote katika kutokuwaruhusu kusafiri.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1001/خطر-الابتعاث-للخارج
- Imechapishwa: 29/12/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1001/خطر-الابتعاث-للخارج
Imechapishwa: 29/12/2025
https://firqatunnajia.com/vijana-wanaotumwa-kusoma-nje-ya-nchi-baadaye-wanakuja-wakiwa-ni-maadui-wa-dini/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket