Swali: Kuna baadhi ya vijana walio na ufahamu wanakuwa na msimamo wa kupita kiasi na baadhi ya mambo ambayo huenda yakawa mshtuko kwa vijana dhaifu wanaohitaji sana mwongozo. Miongoni mwa mambo hayo ni kwamba wanakata kanzu zao kwa ufupi kiasi ambacho kinaweza kufikia kuwa na msimamo mkali?
Jibu: Haya ni mambo madogo na mambo mepesi. Jambo muhimu ni kuwa waepuke kushusha vazi chini ya vifundo. Ikiwa vazi liko kati ya nusu ya muundi mpaka kwenye kifundo cha mguu, basi yote hayo ni yanafaa. Juu yake hadi nusu ya muundi ndiyo ilivyokuja katika Hadiyth:
”Kikoi cha muumini ni hadi kwenye nusu ya muundi.”
Mwisho wake ni mpaka kifundo cha mguu, haipasi kushuka chini ya kifundo. Mradi vazi liko kati ya nusu ya muundi mpaka kifundo, basi hapana kukosoana katika hilo wala halifai kukosoana katika hilo. Bali hilo ni eneo la kufaa; kuanzia nusu ya muundi hadi kifundo. Haijuzu kushusha chini ya vifundo, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Kile kilicho chini ya vifundo katika kikoi kiko Motoni.”
Aidha amewatishia wale wanaoshusha mavazi yao chini ya vifundo vya miguu na akasema kwamba Allaah hatazungumza nao, hatawatakasa na wao watapata adhabu chungu. Kwa hiyo haijuzu kushusha vazi chini ya vifundo. Wala hakuna ubaya ikiwa juu ya vifundo kutoka nusu ya muundi; hapo ndiko mahali pake. Wala haifai kushupalia jambo hili wala kufanya ukakamavu katika hili. Bali inapasa kuwa na upole katika hili na kutomkaripia anayeiinua hadi nusu ya muundi wala kutomkemea ambaye ameiteremsha hadi kwenye kifundo. Si huyu kumkemea huyu wala kinyume chake.
Swali: Vipi kuhusu Hadiyth ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamuru Swahabah kurudia wudhuu´?
Jibu: Hili ni kuhusu kushusha nguo chini ya vifundo vya miguu. Ni jambo limepokelewa katika Hadiyth ambayo ina unyonge. Aidha imepokelewa Hadiyth nyingine inayoonyesha uhalali wa maana hiyo. Lakini makusudio katika hilo ni kutahadharisha dhidi ya kushusha vazi chini ya vifundo, na si kwamba airudie swalah yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamuru kurudia wudhuu´ kwa namna ya ukali na tahadhari. Hakuwaamuru kurudia swalah. Wanazuoni wamesema kwamba lengo katika hili ni onyo dhidi ya kushusha vazi chini ya vifundo na kwamba ni jambo ovu linalopasa kuogopwa kulifanya, khaswa ndani ya swalah.
Swali: Ikiwa kuna mtu ni mshonaji, kisha akamjia mtu akamshurutisha amshonee vazi linaloshuka chini ya vifundo?
Jibu: Anapaswa kumuelekeza mshonaji na amkanye. Asiwashonee chini ya vifundo isipokuwa tu ikiwa makusudio ni kulifanya juu ya vifundo, kisha litakapofuliwa linajikunja na kupanda juu zaidi, kwa sababu baadhi ya vitambaa vinapofuliwa hupanda. Hivyo ikiwa kuna alama ya kushuka chini ya kifundo, waache wakiwa wamelipanua ili baada ya kufuliwa liwe sawasawa. Ikiwa makusudio ni hivyo, basi hakuna tatizo… halafu alinyanyue juu. Endapo kutahitajika kulipunguza literemke, basi alitetemeshe kwa sharti kuwa lisishuke chini ya kifundo cha mguu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/973/لاسبال-بين-الغلو-والتفريط
- Imechapishwa: 29/12/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/973/لاسبال-بين-الغلو-والتفريط
Imechapishwa: 29/12/2025
https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-akijibu-baadhi-ya-maswali-muhimu-kuhusu-isbaal/