Vichinjwa zaidi ya vilivyosuniwa katika ´Aqiyqah

Swali: Ni ipi hukumu mtu akifanya ´Aqiyqah ya vichinjwa vingi zaidi kuliko vile vilivyosuniwa kama mfano wa vichinjwa vinne?

Jibu: Haijuzu kufanya ´Aqiyqah kwa zaidi ya vilivyosuniwa. Lakini vichinjwa vilivyozidi akinuia kula nyama, na si ´Aqiyqah, maneno ya Fuqahaa´ kwamba afanye ´Aqiyqah ya ng´ombe au ngamia, wamesema ikiwa wataonelea kufaa hivo basi bado [kichinjwa hicho] atazingatiwa ni kwa kichwa cha mtu mmoja. Kwa ajili hiyo wakasema bora ni kuchinja kondoo au mbuzi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanz-uth-Thamiyn, uk. 152
  • Imechapishwa: 24/07/2020