Vichinjwa vya Ahl-ul-Kitaab vinavyochinjwa kwa pamoja

Swali: Ni ipi hukumu ya vichinjwa vinavyoletwa kutoka nje ya nchi hii kama mfano wa Brasilia na kwenginepo ambavyo peketi zake zimeandikwa kwamba vimechinjwa kwa njia ya Kishari´ah?

Jibu: Hili ni tatizo. Vimetoka kwa Ahl-ul-Kitaab na msingi ni kwamba vichinjwa vya Ahl-ul-Kitaab ni halali:

وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ

“… na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni halali kwenu.”[1]

Bi maana vichinjwa vyao. Huu ndio msingi. Lakini msingi huu umeingiliwa na jambo ambalo ni kwamba wanachinja ndege hizi kwa pamoja. Wanatumia mashine zilizo na makali ambazo zinakata vichwa vyake kwa wakati mmoja. Hili ndilo tatizo linalotokea juu ya uhalali wake. Kwa ajili hiyo baadhi ya wanachuoni wamelinyamazia. Mara ya kwanza Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) alikuwa akisema kuwa vichinjwa hivyo ni vya Ahl-ul-Kitaab na hivyo ni halali. Lakini alipojua kuwa wanachinja kwa njia hii kwa mpigo mmoja, analinyamazia.

[1] 05:05

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (97) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igatha26-02-1440-h.mp3
  • Imechapishwa: 09/05/2019