Kuongozwa ndani ya swalah na aliyepitwa swalah

Swali: Kuna mtu aliswali pamoja na mkusanyiko na alikuwa amepitwa baadhi ya Rak´ah ambapo akasimama kwa ajili ya kukamilisha zile Rak´ah zilizobaki kwake. Akaja mtu mwingine baada ya swalah ya mkusanyiko kumalizika na akataka kuswali pamoja na mtu huyu aliyepitwa swalah. Ni ipi hukumu ya swalah za wawili hao?

Jibu: Hakuna neno. Inafaa kuongozwa ndani ya swalah na aliyekuja kuchelewa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 09/05/2019