Vibonzo kwenye vyombo vya mawasiliano vya kijamii

Swali: Ni ipi hukumu ya picha za viumbe wenye roho zinazopatikana kwenye kompyuta ambazo hutumiwa na ndugu wanapozungumza kwa kuchati? Vibonzo hivi ukibonyeza kwenye kakichwa ka furaha kanajitokeza na ukibonyeza kwenye kakichwa ka huzuni kanajitokeza.

Jibu: Mambo haya hayana asli katika Shari´ah. Hakuna haja ya kutumia picha ya kiumbe chenye roho isipokuwa kwa dharurah. Jambo hili sio miongoni mwa dharurah. Mambo haya hayana asli katika Shari´ah.

Ikiwa wanahitajiana wanaweza kuwasiliana kwa kutumia njia nyingine.

Ama kuhusiana na nembo za vibonzo hivi vya kuonyesha furaha au huzuni, sio katika mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.cm
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=NSswQgkCxIs
  • Imechapishwa: 04/12/2014