Swali: Unasemaje juu ya kitabu ”Dhwaahir-al-Irjaa´ fiyl-Fikr al-Islaam”? Umependekeza mjeledi wa pili…

Jibu: Ndio, nimekiona. Zaidi ya miaka thalathini iliyopita, wakati nilipokuwa nafundisha katika chuo kikuu [al-Madiynah], nilikaa katika kikao kikubwa na nikaulizwa kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh. Nikasema kuwa ni Suufiyyah wa zama hizi. Na hivi sasa napata kusema kuhusu kundi hili la leo ambalo linaenda kinyume na Salaf – au kama jinsi adh-Dhahabiy huwa akisema: ”Wameenda kinyume na Salaf katika mambo mengi” – na kwamba ni Khawaarij wa zama hizi. Meneno yao yanaafikiana na Khawaarij pindi wanapomfanyia Takfiyr anayetumbukia katika dhambi kubwa. Sijui kama hili pia ni katika moja ya kasoro zao au vitimbi, ninasema hivi kutokana na maneno ya Allaah:

وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَىٰ أَلَّا تَعْدِلُوا ۚاعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ

“Na wala chuki ya watu isikuchocheeni kutokufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu; hivyo ni karibu zaidi na uchaji.” (05:08)

Sijui kama wanasema wazi kuwa kila dhambi kubwa ni kufuru. Hata hivyo wanasema kila wakati kuhusu baadhi ya madhambi makubwa wakati wananyamazia mengine. Kwa ajili hiyo sionelei kuwa mtu aseme kuwa ni Khawaarij moja kwa moja, isipokuwa katika baadhi ya vipengele. Hili ni katika uadilifu ambao tumeamrishwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alalbany.net/fatawa_view.php?id=6546
  • Imechapishwa: 12/12/2014