Swali: Baadhi ya wanafunzi wamesoma Radd yako kwa mheshimiwa Shaykh Bakr Abu Zayd katika Taamam-ul-Minnah na kwamba ni Radd ya kielimu na ya nguvu. Lakini hata hivyo ndani yake kwahakika kuna baadhi ya matamshi ambayo Radd inahitajia, ambayo baadhi ya Ahl-ul-Bid´ah wameyatumia dhidi ya Ahl-us-Sunnah na kudai kwamba Ahl-us-Sunnah wanapigana Radd na kusemana vibaya wao kwa wao. Ili kupiga fikira hizi mbaya kutoka kwa watu hawa wa Bid´ah, tunatarajia unaweza kutubainishia maoni yako kwa Shaykh Bakr Abu Zayd na Radd zake za nguvu na nyingi kwa Ahl-ul-Ahwaa´ kama mfano wa Zaahid al-Kawthariy na mwanafunzi wake mwaminifu anayejinasibisha kwake, al-Ghumaariy, as-Swaabuuniy na wengineo.

Jibu: Tunaonelea kuwa tunajinasibisha kwa Salaf-us-Swaalih na tunatarajia kuwa madai haya ni ya kihakika na ya kweli na sio maneno tu ya bure. Tunajua kuwa Salaf-us-Swaalih walikuwa hawapakani mafuta inapokuja katika haki. Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:

”Hakuna yeyote katika sisi isipokuwa anaraddi na kuraddiwa, isipokuwa aliyemo ndani ya kaburi hili.”

Wakati tunapomraddi muheshimiwa Shaykh Bakr, tunafanya hivo ili kuinusuru Sunnah na sio mtu. Kwa mujibu wa tunavyojua ni mmoja katika ndugu zetu wanaoilinda Sunnah na Manhaj ya Salaf-us-Swaalih na kufuatilia makosa ya Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal. Ninasema haya sio kwa ajili ya kupaka mafuta, bali ninaonelea hivo hakika. Hata hivyo ninaoelea kuwa hilo litanizuia mimi na kutobainisha haki wakati inapokuja katika kumraddi mtu kama mfano wake maadamu ninaolea kuwa amefanya kosa katika yale niliyompa.

Kuhusu baadaye kupatikana watu wenye kutumia hili, ni kitu ambacho hakiwezi kuepukwa. Watu hawa wanawinda kwenye maji machafu. Hata hivyo tuwajulishe watu hawa ya kwamba Ahl-us-Sunnah, hata kama watatofautiana katika baadhi ya mambo ya matawi wana kiigizo kwa hilo kwa hilo kati ya Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na waliokuja baada yao katika karne tatu bora, wana umoja katika misingi na ya Shari´ah na ´Aqiydah. Haidhuru kitu tukitofautianakatika baadhi ya mambo ya matawi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (2)
  • Imechapishwa: 12/12/2014