Vibao vilivyoandikwa (الله) na (محمد) 02

Swali: Mara nyingi tunaona kwenye ukuta kumeandikwa ”Allaah” na pembeni yake jina la ”Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)” au tunayaona hayo kwenye ngozi, vitabu au baadhi ya misahafu. Je, kitu hicho ni sahihi?

Jibu: Mweko huo si sahihi. Kwa sababu hilo linamfanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mwenza wa Allaah na anayelingana Naye. Endapo mtu ataona maandishi haya na hajui wanaoitwa majina hayo basi atayakinisha ya kwamba wanalingana na kufanana. Kwa hiyo ni lazima kuondosha jina la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kubakie jina la ”Allaah” peke yake. Ni neno linalosemwa na Suufiyyah na wanalifanya ni badala ya Dhikr. Wanasema ”Allaah, Allaah, Allaah”. Kutokana na hilo lifutwe pia. Kusiandikwe katika ukuta Allaah wala Muhammad. Wala kusifanywe hivo kwenye viraka wala kitu kingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Manaahiy al-Lafdhwiyyah, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 01/07/2022