Allaah (Subhaanah) amewajibisha Ummah huu uwe na kikosi cha watu kinacholingania kwa Allaah (Ta´ala), kinachowaelekeza watu katika kheri, kinawaamrisha mema na kuwatahadharisha na kuwakataza shari. Amesema (Ta´ala):

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu. Hao ndio waliofaulu.”[1]

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi.”[2]

Kutokana na Aayah hizi tukufu wanazuoni wamethibitisha kwamba kulingania kwa Allaah (Ta´ala) ni faradhi kwa baadhi ya waislamu. Katika kila zama na mahali ni lazima kuwepo kikundi cha waislamu kinacholingania; asipokuweko yeyote anayesimamia kazi hiyo basi wanapata dhambi wote.

[1] 3:104

[2] 16:125

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 8
  • Imechapishwa: 28/07/2022