Kunyanyua mikono na kinachosemwa kati ya Takbiyr za ´iyd

Swali: Je, kuna kitu tunatakiwa kusema kati ya zile Takbiyr za ´iyd? Je, tunyanyue mikono pamoja na kila Takbiyr?

Jibu: Hatunyanyui. Anatakiwa aseme yale yaliyopokelewa kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) – Allaah akitaka “Subhaan Allaah, Alhamdulillaah, Laa ilaaha illa Allaah, Allaahu Akbar”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 176
  • Imechapishwa: 03/07/2022