Swali: Katika kipindi cha mwisho kumedhihiri viatu vya wanawake ambavyo mbele yake ni vyenye kufanana na viatu vya wanaume vilivyo na vidole na nyuma na chini yake vimekaa kama viatu vya wanawake. Ni ipi hukumu yake?

Jibu: Hivi vinaendana na yule Khunthaa ambaye hajulikana ni mwanaume au mwanamke. Ikiwa uinje wake vinaonekana kama viatu vya wanaume na mtu akivivaa basi atafikiria kuwa amevaa viatu vya wanaume, hapo haitofaa kwa mwanamke kuvivaa. Kama ambavyo mwanaume akipata viatu ambavyo uine wake ni kama viatu vya wanawake lakini kwa chini yake ni kama viatu vya wanaume, haitojuzu kwake pia kuvivaa. Kwa sababu kinachozingatiwa ni ule udhahiri.

Nasaha zangu kwa dada zangu ni kwamba wasivae viatu hivi. Jambo ni la khatari. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amewalaani wanaume wenye kujifananisha na wanawake kama ambavyo pia amewalaani wanawake wenye kujifananisha na wanaume.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1452
  • Imechapishwa: 03/01/2020