Swali: Kuna watu wenye kuona uzito kusoma as-Sajdah na al-Insaan katika Fajr ya siku ya ijumaa. Je, yakubaliwe maneno yao?

Jibu: Hapana. Kinachozingatiwa katika kukhafifisha ni ukhafifishaji wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye ndiye kiigizo. Anas anasema:

“Alikuwa akikamilisha na akikhafifisha swalah.”

“Sijamuona imamu anayekhafifisha na kukamilisha swalah kuliko Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Kwa hivyo anatakiwa kuigilizwa katika hili (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye ndiye aliyewafunza watu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23524/حكم-من-يعد-قراءة-السجدة-والانسان-شاقة
  • Imechapishwa: 04/02/2024