75. Athar ”Msimswalie yeyote yule asiyekuwa Mtume… ”

75 – ´Abdullaah bin ´Abdil-Wahhaab ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Ziyaad ametuhadithia: ´Uthmaan bin Hakiym bin ´Abbaad bin Haniyf amenihadithia, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema:

”Msimswalie yeyote yule asiyekuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini waislamu wa kiume na waislamu wa kike wanaombewa msamaha.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Wapokezi wake ni waaminifu. Udhahiri ni kuwa ´Abdur-Rahmaan bin Ziyaad ni ar-Raswaaswiy. Ibn Abiy Haatim (2/2/235) ameeleza kwamba baba yake amesema kuwa ni mwenye kuaminika.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 69
  • Imechapishwa: 04/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy