74. Athar ”Hakuna du´aa yoyote ambayo mwanzo wake… ”

74 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: ´Amr bin Musaafir ametuhadithia: Mzee mmoja wa familia yangu amenihadithia: Nimemsikia Sa´iyd bin al-Musayyab akisema:

”Hakuna du´aa yoyote ambayo mwanzo wake haswaliwi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), isipokuwa inakuwa yenye kuning´inizwa kati ya mbingu na ardhi.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni dhaifu.  al-Bukhaariy amesema kuwa ´Amr bin Musaafir – ambaye pia anaitwa ´Amr bin Musaawir, na hili la pili ndio sahihi kama ilivyo katika ”al-Miyzaan” – anasimulia Hadiyth munkari, ilihali Abu Haatim amesema kuwa ni mnyonge. Isitoshe mzee anayetokana na familia yake hakumtaja jina. ash-Sakhaawiy amepokea Athar hiyo kupitia kwa ´Abdullaah bin ´Umar na akasema:

”Ameipokea Ibn Maniy´ katika ”al-Musnad” yake, mjukuu wake, al-Baghawiy katika ”al-Fawaa-id” na, kupitia kwake, an-Numayriy kwa cheni ya wapokezi dhaifu.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 68-69
  • Imechapishwa: 04/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy