Bora kumtoa swadaqah au kumla mnyama niliyemuokota?

Swali: Kuhusiana na mnyama hoa aliyepotea baada ya kupita muda na kumtangaza bora ni kumtoa swadaqah au kumchukua na kumla?

Jibu: Hapana, ni milki yako:

“Ni wako, wa ndugu yako au wa mnyama mwitu.”

Lakini baada ya kumtangaza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote anayemuhifadhi mnyama aliyepotea basi amepotea muda wa kuwa hajamtangaza.”

Ameipokea Muslim.

Anatakiwa kumtangaza mwaka mzima. Ikiwa ni vigumu kumuhifadhi basi amuuze, ahifadhi ile thamani yake na sifa zake. Ikiwezekana kumchunga pamoja na wanyama wake wengine basi amchunge.

Swali: Lakini amtoe swadaqah au ammiliki?

Jibu: Sio milki yake. Ukitimia mwaka ndio milki yake. Mpaka pale atakapokuja mmiliki wake siku miongoni mwa siku atamkabidhi akimweleza kwa mujibu wa sifa zake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23525/حكم-ضالة-الغنم-بعد-مضي-الوقت-وتعريفها
  • Imechapishwa: 04/02/2024