Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
عن الزبير بن عدي، قَالَ: أتينا أنسَ بن مالك رضي الله عنه فشكونا إِلَيْه مَا نلقى مِنَ الحَجَّاجِ. فَقَالَ: (اصْبرُوا؛ فَإنَّهُ لا يَأتي عَلَيْكُم زَمَانٌ إلا والَّذِي بَعدَهُ شَرٌّ مِنهُ حَتَّى تَلقَوا رَبَّكُمْ) سَمِعتُهُ مِنْ نَبِيِّكُمْ صلى الله عليه وسلم. رواه البخاري
92 – az-Zubayr bin ´Adiyy (Radhiya Allaahu ‘anh) amesema: “Kuna watu walimjia Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) na kumshtakia yanayowasibu kutoka kwa al-Hajjaaj. Akawaambia: “Kuweni na subira. Kwani hakutokuja zama isipokuwa ilio baada yake ni yenye shari zaidi kuliko iliyokutwa [hali itaendelea kuwa hivo] mpaka mkutane na Mola Wenu.” Nimeyasikia hayo kutoka kwa Mtume wenu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Ameipokea al-Bukhaariy
Katika Hadiyth hii kuna uwajibu wa kuwa na subira kwa watawala. Haijalishi kitu hata kama watadhulumu na kufanya ukandamizi. Kwa sababu kuna wakati wewe na wao mtasimama na nyote mkiwa sawasawa. Hapa ni mbele ya Mfalme wa wafalme. Utakuwa mgombezi wao siku ya Qiyaamah wakikudhulumu. Usifikiri kuwa dhuluma inayopatikana duniani itaondoka hivihivi. Hapana. Haki ya kiumbe ni lazima ilipwe siku ya Qiyaamah. Wewe utasimama na wao siku ya Qiyaamah mbele ya Allaah ili awahukumu kwa uadilifu. Hivyo, kuwa na subira na usubiri faraja. Kwa hilo utapata utulivu wa nafsi na uthabiti. Kusubiri faraja ni ´ibaadah unayomuabudu Allaah kwayo. Hivyo subiri faraja kutoka kwa Allaah.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/38)
- Imechapishwa: 17/10/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)