Swali: Kuwinda kenge kwa kumwaga maji au kutoa moshi wa gari kwenye mashimo yao…

Jibu: Haijuzu. Wengi wa watu wanawinda kenge sio kwa ajili ya kumla, kwa ajili ya burudani. Matokeo yake wanamuadhibu mnyama huyu. Haijuzu kufanya hivo. Ni kweli kwamba inafaa kula nyama ya kenge, lakini yule anayewatesa kwa ajili ya burudani au kwa ajili ya kucheza anapaswa kutambua kuwa wanyama wa heshima yao, wanaliwa na kunyiwa na mfano wa hayo. Inafaa kwake kuwakamata tu kwa ajili ya kuwala, na sio kwa ajili ya burudani au kupoteza muda. Baadhi wanayajaza magari yamejaa kenge, sio kwa ajli ya kuwala, bali kwa ajili tu ya kujipa faraja. Ni haramu kufanya hivo. Aidha haijuzu kuwaua kenge kwa njia hii, kukiwemo kwa kutumia gesi ya gari. Haijuzu kufanya hivo. Ni wanyama walio na roho, na kwa ajili hiyo haifai kuwaadhibu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 01/12/2023