Dr Ibraahiym [ar-Ruhayliy] amesema:

”Ahl-ul-Bid´ah ni wale ambao wameenda kinyume na ´Aqiydah na mfumo wa Ahl-us-Sunnah katika kujengea dalili, kufunza, usomaji, kulingania kwa Allaah, wakafuata matamanio na hawakuwafuata wanazuoni wa Ahl-us-Sunnah. Bali wanawadharau, wanawatukana na kujiona wao ni bora kuwaliko. Hawa ndio wazushi na wapotofu.”

Kupitia utambulisho huu mrefu anachopata kufahamu mtu ni kwamba mtu au kundi hawawi wazushi wala wapotofu isipokuwa wanapokusanyikiwa na mambo yote haya. Utambulisho huu ni wa ajabu na ni uthibtisho wa ajabu ambao unapingana na misingi, mfumo na hukumu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

1 – Khawaarij ambao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewasimanga na akaamrishwa wapigwe vita, ambapo wakapigwa vita na Maswahabah na wakawaua wengi wao, walikuwa hawana isipokuwa kosa moja; walikuwa wakikufurisha kwa hukumu na madhambi makubwa. Hawakuwa wakishirikisha katika uola wa Allaah, walikuwa hawamwabudu mwengine isipokuwa Allaah pekee na hawakua wakikanusha majina na sifa za Allaah. Muda ulivyoenda ndipo wakaanza kuwa na ´Aqiydah za Jahmiyyah na Mu´tazilah. Bali wengi wao wakaanza mpaka kuyaabudia makaburi.

2 –  Salaf hawakushurutisha sharti zilizowekwa na Dr Ibraahiym ili kumzingatia mtu kuwa ni mzushi. Bali walikuwa wakifanya Tabdiy´ na pengine wakafikia kukufurisha kwa sababu ya jambo limoja tu linalohusu ´Aqiydah. Waliwakufurisha wale Qadariyyah waliyopindua kwa sababu ya kukanusha kwao elimi elimu ya Allaah ya milele. Wa kwanza aliyewakufurisha alikuwa ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye alisema:

”Naapa kwa ambaye nafsi ya Ibn ´Umar iko mikononi Mwake! Lau mmoja wao angelitoa dhahabu mfano wa mlima wa Uhud, basi Allaah asingeikubali kutoka kwake mpaka aamini Qadar. Ukikutana na watu hao, basi waeleze kwamba mimi niko mbali kabisa nao na kwamba wao wako mbali kabisa nami.”[1]

Swahabah mtukufu ´Ubaadah bin as-Swaamit (Radhiya Allaahu ´anh) amesema maneno mfano wa hayo.

Wakati Qadariyyah waliyokuja nyuma walipobadili ´Aqiydah yao na baadaye wakathibitisha elimu lakini wakakanusha matakwa ya Allaah juu ya matendo ya waja, ndipo wanazuoni wakatofautiana juu yao ambapo baadhi wakawakufurisha na wengine wakawafanyia Tabdiy´.

Wakati Mu´tazilah waliposema kuwa mtenda dhambi sio kafiri wala muislamu, wakawafanyia Tabdiy´ na kuwapa jina la ”Mu´tazilah”.

Wakati Ahl-ul-Ahwaa´ waliposema kuwa Qur-aan ni kiumbe na sio maneno ya Allaah, wanazuoni wa Ahl-us-Sunnah waliwakufurisha.

Wakati baadhi ya wanazuoni wa Ahl-ul-us-Sunnah waliposema kuwa matamshi yao ya Qur-aan yameumbwa, wanazuoni wa Ahl-us-Sunnah waliwafanyia Tabdiy´.

Wakati Murji-ah walipopotea juu ya utambulisho wa imani, wakayaondosha matendo katika imani na wakasema kuwa haizidi na wala haipungui, Ahl-ul-us-Sunnah waliwafanyia Tabdiy´.

Wakati baadhi yao waliposema kuwa imani ni kule kutambua ndani ya moyo, waliwakufurisha na wakasema kuwa Jahmiyyah waliyopindukia.

Dr Ibraahiym amesema:

”Hiki ndio kipambanuzi kati ya Ahl-us-Sunnah na Ahl-ul-Bid´ah. Hapa ndipo ataona mwenye akili sababu ya maimamu kutowafanyia Tabdiy´ baadhi ya wanazuoni wa Ahl-us-Sunnah licha ya kuafikiana na Ahl-ul-Bid´ah katika baadhi ya mambo.”

Salaf waliwafanyia Tabdiy´ wanazuoni wengi ambao walikuwa ni katika wanazuoni wakubwa wa Ahl-us-Sunnah kwa sababu tu ya kusema kwao kuwa matamshi yao ya Qur-aan ni kiumbe ingawa waliafikiana na Ahl-us-Sunnah juu ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah, tofauti na wanavoona Ahl-ul-Bid´ah. Suala hili ni sehemu tu ya mambo , kama unavoona mwenyewe.

[1] Muslim (8).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan maa fiy Naswiyhati Ibraahiym ar-Ruhayliy min al-Khalal wal-Ikhlaal, uk. 79-81
  • Imechapishwa: 10/12/2022