Usisome kwa wasiokuwa wanachuoni

Swali: Ni yapi maoni yako kwa mwanamke kusoma kupitia mwanafunzi pasi na wanachuoni?

Jibu: Asiyekuwa na kitu hawezi kutoa kitu. Vipi utasoma kwa wasiokuwa wanachuoni? Haiwezekani. Maadamu wewe mwenyewe umemsifu kuwa sio katika wanachuoni haiwezekani kusoma kwake. Kwa kuwa elimu inachukuliwa kutoka kwa watu wake ambao ni wanachuoni. Inachukuliwa kutoka kwenye vifua vya wanachuoni. Vipi basi utasoma kwa mtu asiyekuwa mwanachuoni? Asiyekuwa mwanachuoni ina maana ni mjinga. Haiwezekani mtu akasoma kwa mjinga. Ni lazima mtu awe anasifika kuwa na elimu. Elimu ya Kishari´ah ni ile inayochukuliwa kutoka kwenye Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imejengwa juu ya dalili. Elimu inakuwa imejengwa juu ya dalili: Allaah Amesema kadhaa na Mtume amesema kadhaa. Ikiwa anasifika kuwa sio katika wanachuoni, huyu inatakiwa kuachana naye na kumtenga. Mjinga anaharibu zaidi kuliko anavyotengeneza.

Check Also

Darsa na al-Fawzaan au kazi?

Swali: Mimi ni mara yangu ya kwanza ninakaa katika darsa hizi zilizobarikiwa. Kwa kweli nataka …