Usifasiri Aayah yoyote kabla ya kurejea katika vitabu vya tafsiri ya Qur-aan

Swali: Je, inajuzu kwa mtu kufasiri baadhi ya Aayah ambazo maana yake iko wazi pasi na kurejea katika vitabu vya tafsiyr ya Qur-aan?

Jibu: Hapana, anaweza kuwa ni mwenye kukosea katika kuifasiri. Ni lazima kurejea katika vitabu vya tafsiyr vinavyoaminika. Wewe unazungumzia kwa muradi wa Allaah. Unasema muradi wa Allaah kuhusiana na Aayah hii ni kadhaa. Wewe unaeleza juu ya Allaah. Unasema kuhusu Allaah. Ukisema kuhusu Allaah pasi na elimu unapata dhambi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (69) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-05-28.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020