Swali: Mimi ni mwanafunzi mwanamke na ninauliza natakiwa kuwa na msimamo gani kwa mlinganizi mwanamke anayesema kuwa ni Salafiyyah na wakati huohuo anashaji´isha kutomtakia rehema Imaam an-Nawawiy na kuchoma moto kitabu “Tafsiyr-ul-Jalaalayn”. Je, nichukue elimu kutoka kwake…
Jibu: Huyu ni mwenye kupetuka mipaka. Huyu ni mwenye kupetuka mipaka. Usimuige na wala usichukue elimu kutoka kwake. Huku ni kupetuka mipaka.
Imaam an-Nawawiy ni imamu mtukufu.
Kitabu “Tafsiyr-ul-Jalaalayn” kina manufaa na ndani yake mna faida nyingi hata kama baadhi ya sifa zimepindishwa maana. Ni chenye kukubaliwa kwa wanachuoni. Watunzi hawa wawili walikuwa ni maimamu watukufu; as-Suyuutwiy na al-Mahilliy. Ni katika maimamu wenye kujulikana.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=155707
- Imechapishwa: 30/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)