Swali: Mimi ni mwanafunzi mwanamke na ninauliza natakiwa kuwa na msimamo gani kwa mlinganizi mwanamke anayesema kuwa ni Salafiyyah na wakati huohuo anashaji´isha kutomtakia rehema Imaam an-Nawawiy na kuchoma moto kitabu “Tafsiyr-ul-Jalaalayn”. Je, nichukue elimu kutoka kwake…

Jibu: Huyu ni mwenye kupetuka mipaka. Huyu ni mwenye kupetuka mipaka. Usimuige na wala usichukue elimu kutoka kwake. Huku ni kupetuka mipaka.

Imaam an-Nawawiy ni imamu mtukufu.

Kitabu “Tafsiyr-ul-Jalaalayn” kina manufaa na ndani yake mna faida nyingi hata kama baadhi ya sifa zimepindishwa maana. Ni chenye kukubaliwa kwa wanachuoni. Watunzi hawa wawili walikuwa ni maimamu watukufu; as-Suyuutwiy na al-Mahilliy. Ni katika maimamu wenye kujulikana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=155707
  • Imechapishwa: 30/08/2020