Usiache matendo mema kwa kuogopa watu

Swali: Je, inafaa kuacha kufanya matendo kwa kuogopa kuonekana?

Jibu: Huo ni wasiwasi kutoka kwa shaytwaan. Nimetaka kuzindua jambo hilo lakini nimesahau. Baadhi ya watu huacha kufanya matendo mema, wakaacha kusimama usiku kuswali wakafikia kuacha mpaka swalah za mkusanyiko eti kwa sababu wanaogopa wasije kuonekana. Hilo linatokana na shaytwaan. Unapaswa kufanya matendo mema, mtakasie nia Allaah (´Azza wa Jall) na mtake msaada Allaah kutokana na shaytwaan. Lakini kuacha kufanya matendo mema kwa sababu ya kuogopa kuonekana… imekuja katika Athar:

“Kutenda kwa ajili ya watu ni shirki, na kuacha kutenda matendo kwa ajili ya watu pia ni shirki.”

Fanya matendo mema mtake msaada Allaah kutokana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali.

Wakati mwingine shaytwaan anakushawishi usitoe swadaqah na kwamba eti watu watakutuhumu unataka kujionyesha na unafiki. Hilo linatokana na shaytwaan. Achana nalo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (05)
  • Imechapishwa: 20/02/2024