104. Hadiyth ”Mtume wa Allaah alimsikia bwana mmoja akiomba du´aa katika swalah yake… ”

106 – Muhammad bin Abiy Bakr ametuhadithia: ´Abdullaah bin Yaziyd ametuhadithia: Haywah amenihadithia: Abu Haaniy’ Humayd bin Haaniy’ amenikhabarisha: Abu ´Aliy ´Amr bin Maalik amemuhadithia kuwa amemsikia Fadhwaalah bin ´Ubayd, Swahabah wa Mtume wa Allaah (Swaalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akisema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimsikia bwana mmoja akiomba du´aa katika swalah yake pasi na kumtukuza Allaah wala kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Huyu amefanya haraka.” Kisha akamwita na kumwambia yeye au mwengine: ”Anaposwali mmoja wenu, basi aanze kwa kumtukuza Allaah na kumsifu, halafu amswalie Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha baadaye aombe anayoyataka.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni nzuri. Wapokezi wake wote ni waaminifu na ni wanamme wa Muslim. Isipokuwa tu ´Amr bin Maalik an-Nukriy, ambaye ni mwaminifu kama alivosema adh-Dhahabiy. Haafidhw Ibn Hajar amesema kuwa ni mwenye kuaminika na anakosea. Haywah ni Ibn Shurayh. Abu ´Abdir-Rahmaan ´Abdullaah bin Yaziyd ni al-Muqriy’. Kupitia kwake amepokea Imaam Ahmad (6/18) na wengineo. at-Tirmidhiy pia ameipokea na akasema kuwa ni nzuri na Swahiyh. al-Haakim naye ameipokea na akasema kuwa ni Swahiyh na ni kwa mujibu wa sharti za Muslim. adh-Dhahabiy ameafikiana naye. Ni jambo ambalo haifichiki kuwa linatakiwa kuangaliwa vyema. an-Nasaa´iy ameipokea kupitia kwa Ibn Wahb, kutoka kwa Abu Haaniy’.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 88
  • Imechapishwa: 20/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy