Swali: Tumekusikia ukisema kuwa ambaye hakatazi maovu kwa moyo wake hana imani yoyote. Je, anakuwa kafiri? Hili ni kuhusu maovu yote au ovu moja tu?

Jibu: Ambaye hakatazi maovu kwa moyo wake hana imani yoyote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye kasema hivo:

”Na hakuna nyuma ya hilo imani yoyote sawa na punje ya hardali.”[1]

Usipekue kaisi cha imani yake. Haifai kupekua na kudharau Hadiyth za makemeo. Pengine hana imani kabisa  – Allaah ndiye anayejua zaidi.

[1] Muslim (50).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (05)
  • Imechapishwa: 20/02/2024