107 – Muhammad bin al-Muthannaa ametuhadithia: Mu´aadh bin Hishaam ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Haarith, ambaye amesema:
”Abu Haliymah Mu´aadh alikuwa akimswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Qunuut.”[1]
Mwisho. Himdi zote njema anastahiki Allaah pekee. Swalah na amani zimwendee bwana wetu Muhammad na jamaa zake[2].
[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Abu Haliymah alikuwa ni Mu´aadh bin al-Haarith al-Answaariy al-Qaariy’. Ibn Abiy Haatim amesema:
”Yeye ndiye ambaye aliteuliwa na ´Umar kama imamu kuwaswalisha watu Tarawiyh katika mwezi wa Ramadhaan.”
Abuul-Waliyd ´Abdullaah bin al-Haarith ni al-Baswriy, ni mwaminifu na ni mmoja katika wanamme wa al-Bukhaariy na Muslim. Ibn Naswr ameipokea kwa tamko lisemalo:
”Alikuwa akisimama katika Qunuut ndani ya Ramadhaan akiomba du´aa, akimswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akiomba du´aa ya kunyesha mvua.” (Qiyaam-ul-Layl, uk. 136)
Tazama “Swalaat-ut-Taraawiyh”, ya al-Albaaniy, humo mna hukumu nyingi zinazofungamana na ´ibaadah hii.
[2] Mpaka hapa tunamaliza kuhakiki na kukiwekea maelezo kitabu hiki kilichobarikiwa. Kimemalizwa mchana wa 7 Rabiy´-ul-Awwal 1382 Dameski. Himdi zote njema zinamstahikia Allaah pekee. Swalah na amani zimwendee yule ambaye hakuna Nabii mwingine baada yake. Kisha nikakipitia kwa mara nyingine, nikaongeza faida kadhaa na nikasahihisha baadhi ya makosa ya uchapishaji. Himdi zote ni za Allaah juu ya mawafikisho Yake.
Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Beirut, 1 Radjab 1389.
- Muhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 88-90
- Imechapishwa: 21/02/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
107 – Muhammad bin al-Muthannaa ametuhadithia: Mu´aadh bin Hishaam ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Haarith, ambaye amesema:
”Abu Haliymah Mu´aadh alikuwa akimswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Qunuut.”[1]
Mwisho. Himdi zote njema anastahiki Allaah pekee. Swalah na amani zimwendee bwana wetu Muhammad na jamaa zake[2].
[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Abu Haliymah alikuwa ni Mu´aadh bin al-Haarith al-Answaariy al-Qaariy’. Ibn Abiy Haatim amesema:
”Yeye ndiye ambaye aliteuliwa na ´Umar kama imamu kuwaswalisha watu Tarawiyh katika mwezi wa Ramadhaan.”
Abuul-Waliyd ´Abdullaah bin al-Haarith ni al-Baswriy, ni mwaminifu na ni mmoja katika wanamme wa al-Bukhaariy na Muslim. Ibn Naswr ameipokea kwa tamko lisemalo:
”Alikuwa akisimama katika Qunuut ndani ya Ramadhaan akiomba du´aa, akimswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akiomba du´aa ya kunyesha mvua.” (Qiyaam-ul-Layl, uk. 136)
Tazama “Swalaat-ut-Taraawiyh”, ya al-Albaaniy, humo mna hukumu nyingi zinazofungamana na ´ibaadah hii.
[2] Mpaka hapa tunamaliza kuhakiki na kukiwekea maelezo kitabu hiki kilichobarikiwa. Kimemalizwa mchana wa 7 Rabiy´-ul-Awwal 1382 Dameski. Himdi zote njema zinamstahikia Allaah pekee. Swalah na amani zimwendee yule ambaye hakuna Nabii mwingine baada yake. Kisha nikakipitia kwa mara nyingine, nikaongeza faida kadhaa na nikasahihisha baadhi ya makosa ya uchapishaji. Himdi zote ni za Allaah juu ya mawafikisho Yake.
Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Beirut, 1 Radjab 1389.
Muhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 88-90
Imechapishwa: 21/02/2024
Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/105-athar-abu-haliymah-muaadh-alikuwa-akimswalia-mtume/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)