Urejeshaji wa pesa zilizowekezwa

Swali: Nikimpa mtu kiwango cha pesa ambacho atakiwekeza katika kitu na baadaye akafilisika, analazimika kuzilipa pesa hizo?

Jibu: Hapana. Ulimwamini juu ya kazi hiyo na hivyo hutakiwi kumtaka azilipe. Jambo la kupata faida na kufilisika haliko mkononi mwake, anaweza kupata faida na anaweza kufilisika. Ni vipi utamtaka kuzilipa?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (30)
  • Imechapishwa: 18/02/2022