3621 – Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Watu aina tatu Allaah hatowatazama siku ya Qiyaamah na wala hawatowasemeza na watakuwa na adhabu yenye kuumiza: Mtu ambaye anaachia maji yatoke katika ardhi tambarare na yanawazuia wapita njia, mtu ambaye anamuuzia mwingine bidhaa baada ya ´Aswr na akamuapia kwa Allaah kwamba ameinunua kwa bei fulani ambapo akamsadikisha ilihali uhalisia ni kinyume na hivo na mtu mwenye kula kiapo kwa kiongozi na hakufanya hivo isipokuwa ni kwa sababu ya malengo ya kidunia; akimpa kitu, basi anatekeleza, na asipompa chochote, hatekelezi.”

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na tamko ni lake, at-Tirmidhiy, Abu Daawuud, Ibn Maajah, Ahmad, Ibn Mandah katika “al-Iymaan”, at-Twahaawiy katika “Mushkil-ul-Aathaar”, al-Bayhaqiy katika “al-Asmaa’ was-Swifaat” na al-Kharaa-itwiy katika “Masaawiy-ul-Akhlaaq”.

Kuhusu nukuu ya mfanya taaliki wa ”al-Ihsaan” juu ya kupindisha sifa ya maneno na kuonekana kwa Allaah (Ta´ala) kwamba maana yake ni kuridhia, kuwapuuza na mfano wake, ni upindishaji wenye kusemwa vibaya unaoenda kinyume na ´Aqiydah ya Salaf. Kimsingi ni kwamba zinatakiwa kupitishwa juu ya udhahiri wake kwa njia inayolingana na ukubwa na utukufu wa Allaah, kama ilivyo katika maneno Yake (Subhaanah):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]

[1] 42:11

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (7/3/1636)
  • Imechapishwa: 08/08/2020