Unyonyeshaji wa chini ya mara tano hauharamishi kuoana

Swali: Kijana anataka kumuoa msichana. Msichana ana kaka anayemzidi mwaka mmoja. Mama wa msichana alimyonyesha kijana huyo mara moja tu siku moja pamoja na mwanawe mkubwa. Je, ndoa kati yao ni sahihi?

Jibu: Unyonyaji wa mara moja haufanyi haramu kuoana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Unyonyaji wa mara moja haufanyi haramu wala unyonyaji wa mara mbili.”

Ni lazima iwe unyonyeshaji wa mara tano ndani ya miaka miwili. Ikiwa kunyonya ni chini ya hapo, na jambo hilo ni lenye uhakika, basi hakupatikani uharamu wa ndoa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1309/عدد-الرضعات-التي-يحرم-بها-النكاح
  • Imechapishwa: 21/06/2026