Swali: Ikiwa mtu ataswali mbele ya imamu katika msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Madiynah kwa sababu kwa mfano msongamano?

Jibu: Haijuzu kuswali mbele ya imamu. Maoni sahihi ni kuwa haijuzu, bali mtu awe nyuma ya imamu. Baadhi ya wanazuoni wanasema inajuzu kutokana na dharurah. Ikiwa ni kutokana na dharurah, basi swalah yake inasihi. Lakini inapasa wazuiwe kufanya hivyo. Inapasa wawe nyuma ya imamu, kulia kwake au kushoto kwake, na si mbele yake. Hivi ndivyo inavyopasa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1325/حكم-التقدم-على-الامام-حال-الزحام
  • Imechapishwa: 21/06/2026