Kumuomba Allaah kwa nuru ya uso Wake

Swali: Vipi ikiwa mtu atasema: ”Ninakuomba kwa nuru ya uso Wako uliong’aa”?

Jibu: Hakuna ubaya. Hili limetajwa katika baadhi ya Hadiyth: ”Ninakuomba kwa nuru ya uso Wako iliyoang’aza mbingu na ardhi.” Hakuna tatizo katika hilo. Nuru Yake ni kubwa, kwayo dunia imeangaza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1326/حكم-قول-اسالك-بنور-وجهك-الذي-اشرقت-له
  • Imechapishwa: 21/06/2026