Ni vipi inakuwa du´aa ya istikhaarah?

Swali: Ni vipi inakuwa du´aa ya istikhaarah?

Jibu: Ni Sunnah. Istikhaarah ni Sunnah. Imetajwa katika Hadiyth ya Jaabir iliyopo katika Riyaadh-us-Swaalihiyn. Lau ungekuwa unasoma Riyaadh-us-Swaalihiyn. Hadiyth ya Jaabir ni Swahiyh. Mtu anapokusudia jambo lisilo la faradhi na akawa ana hali ya kusita juu yake, basi ataomba istikhaarah kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) na ataomba ile du´aa inayojulikana katika Hadiyth ya Jaabir iliyopo katika ”as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na imetajwa katika Riyaadh-us-Swaalihiyn na katika vitabu vingine.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1327/ما-دعاء-الاستخارة
  • Imechapishwa: 21/06/2026