Unaweza kuwaswalia wasiokuwa Mitume?

Swali: Je, inajuzu kumswalia, kwa wasiokuwa Mitume, fulani (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu mwanamke alimwambia mwanamke:

“Niswalie mimi na mume wangu”?

Jibu: Inajuzu kuwaswalia baadhi ya waumini. Lakini hata hivyo hili lisifanywe ndio mazowea kama wafanyavyo Raafidhhwah. Wao wanamkhusisha ´Aliy na kusema “´alayhis-Salaam” au “´alayhis-Swalaatu was-Salaam”. Ikiwa hii ni alama ya Ahl-ul-Bid´ah haijuzu kufanya hivi. Ama mtu akisema hivo baadhi ya nyakati pasi na kufanya ndio mazowea yake ni sawa.

Check Also

Wewe usiwe wa kwanza kumsalimia kafiri

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu kuanza kumsalimia kafiri? Jibu: Haijuzu. Ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu …