Unataka mtawala mzuri? wako wapi sasa raia wazuri!

Watu wengi wanataka viongozi wao wawe wakamilifu kabisa kiasi wanavyoweza. Bila ya shaka tunataka hivi. Tunataka watawala wawe wakamilifu kiasa na wanavyoweza. Lakini hata hivyo sisi hatutangamani nao kikamilifu kiasi na tunavyoweza. Kwa msemo mwingine baadhi ya raia wanataka watawala wawe wakamilifu kiasi na wanavyoweza na wakati rai wao wenyewe ni wapungufu kiasi na inavyowezekana! Je, huu ni uadilifu? Ninaapa kwa Allaah ya kwamba sio uadilifu. Ikiwa unataka upewe haki kikamilifu na wewe unatakiwa kutoa haki ilio juu yako kikamilifu. Vinginevyo hutakiwi kuomba kitu.

Katika hekima ya Allaah (´Azza wa Jall) ni kwamba watawala wanakuwa kama jinsi raia wanavokuwa. Ni hekima mtawala kuwa kama jinsi raia walivo. Akiwa bora, wanakuwa wabora. Akiwa mbaya, wanakuwa wabaya. Katika upokezi:

“Kama mtavyokuwa ndivyo mtavyotawaliwa.”

Ina maana ya kwamba mtawala anawaongoza watu kutokana na hali zao. Mapokezi haya hata kama sio sahihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata hivyo yana maana sahihi. Soma Kauli ya Allaah:

وَكَذَٰلِكَ نُوَلِّي بَعْضَ الظَّالِمِينَ بَعْضًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ

“Na namna hiyo Tunavyowaelekeza baadhi ya madhalimu kuwa marafiki wao kwa wao, kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.” (06:129)

Raia wakiwa madhalimu watawala wanawaendea juu. Raia wakiwa wazuri watawala na wao pia wanakuwa wazuri na kinyume chake. Ikiwa mtawala ni mzuri raia na wao pia wanakuwa wazuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahryi (51 A)
  • Imechapishwa: 23/04/2015