Hakuna viongozi kama viongozi wa Saudia – hakuna wananchi kama wananchi wa Saudia

Tunataka serikali itufanyie kila kile tunachokitaka na iwe kama serikali ya wakati wa makhaliyfah waongofu. Lakini tukiziangalia nafsi zetu tunaona kuwa sisi wenyewe tuna mapungufu.

Kwanza tuna mapungufu katika haki ya Allaah (´Azza wa Jall). Tunasema uongo. Khiyana.

Tuna mapungufu katika wajibu. Je, si kweli? Tunashuhudia juu ya nafsi zetu hili. Tuna yote haya. Vivyo hivyo tuna mapungufu katika mafungamano na nchi. Ni wangapi ambao wanaidanganya nchi na wanayapitisha mambo nyuma yake na wanaficha yale ambayo nchi inawataka wayadhihirishe! Hili ni jambo linajua kila mtu.

Je, huu ni uadilifu kwetu sisi kuitaka serikali kufanya kila inachoweza ili iwe kama zama za makhaliyfah wakati sisi wenyewe tuko kinyume? Hapana. Hili linaingia katika Kauli ya Allaah:

الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ

“Ambao wanapojipimia kwa watu, basi wapimiwe kamilifu. Lakini wanapowapimia wengine au kwa mizani, basi wao wanapunguza.” (83:02-03)

Sisi tunatarajia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) atuongoze sisi na serikali yetu katika haki na atengeneze mambo yao.

Sisi tunajua kuwa hakuna nchi yoyote katika uso wa ardhi ilio na watawala kama watawala wetu – pamoja na mapungufu walio nayo – na kuwa hakuna wananchi ambao wanawakilisha Uislamu na Tawhiyd kihakika kama jinsi wanavofanya wananchi wa Saudi Arabia – pamoja na mapungufu walio nayo. Sisi hatusemi haya kwa sababu ya ufanaa na ushabiki. Lakini tunasikia na kusoma kuhusu nchi zingine. Ni wajibu kwetu tuwe waadilifu. Toa na uchukue. Ama kuchukua tu bila ya kutoa, bila ya shaka hili ni kupotoka na jeuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahryi (51 A)
  • Imechapishwa: 23/04/2015