Kosa la kwanza la jumla katika tafsiri ya Qur-aan ya as-Swaabuuniy “Swafwat-ut-Tafaasiyr” ni kwamba ameijenga juu ya marejeleo yasiyopendekezwa pamoja na kuwa anasema kuwa ni katika tafsiri za Qur-aan ambazo ni sahihi zaidi. Mfano wa vitabu hivyo ni “Talkhiys-ul-Bayaan” ya ar-Radhwiy ambaye alikuwa Shiy´iy, Raafidhwiy na Mu´taziliy, “al-Khashshaaf” ya az-Zamakhshariy ambaye alikuwa Mu´taziliy, tafsiri ya Ashaa´irah kama ar-Raaziy, Abus-Su´uud, tafsiri ya as-Saawiy na al-Baydhwaawiy na baadhi ya fasiri za Qur-aan za leo kama ya Sayyid Qutwub na al-Qaasimiy. Ni dhahiri ya kwamba haya yanawadanganya wasomaji ambao hawajui haki kuhusu vitabu hivi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayân li Akhtwaa’ Ba´dhw-il-Kuttaab, uk. 59
  • Imechapishwa: 23/04/2015