Katika ukurasa wa 195 na 395 anakariri – Muhammad ´Aliy as-Swaabuuniy – neno “shahidi wa Kiislamu” na anakusudia Sayyid Qutwub (Rahimahu Allaah) wakati anapomnukuu ili kufasiri baadhi ya Aayah. Hii ni kwa kuzingatia ya kwamba haijuzu kumshuhudilia shahaadah yeyote midhali hakuna dalili ya hilo katika maneno ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hatumshuhudilii Pepo yeyote bila ya dalili. Hata hivyo tunatarajia mema kwa waislamu ambao wanafanya matendo mazuri na kuchelea kwa waislamu wanaotenda madhambi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan li Akhtwaa’ Ba´dhw-il-Kuttaab, uk. 64
  • Imechapishwa: 23/04/2015