Ndio maana Ibn Khuyzamah alikuwa anaitwa imamu wa maimamu

Mwandishi amemsifu Ibn Khuzaymah na kusema:

“… na mtu ambaye alikuwa anaitwa “Imamu wa maimamu katika wakati wake”.”

Amemtaja Ibn Khuzaymah kama “Imamu wa maimamu”. Kwa sababu wanachuoni wengi katika wakati wake walikuwa ni wanafunzi wake. Wote wamekuja kutoka kwake. Allaah amjaze kheri! Alikuwa ni miongoni mwa wale wakubwa waliokuwa wamehifadhi Sunnah na mmoja katika Fuqahaa´ wakubwa katika Sunnah na maimamu wake. Yeye ndiye mwenye kauli ambayo ni maarufu:

“Sunnah haigongani. Mwenye kuona kwamba Hadiyth mbili zinagongana azilete kwangu ili nimuoanishie nazo.”

Inatokana na ufahamu wake wa kina. Allaah amjaza kheri.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 349
  • Imechapishwa: 23/04/2015