Unasemaje juu ya kulijipua kwa kujitoa muhanga Palestina?

Swali: Unasemaje juu ya kulijipua kwa kujitoa muhanga Palestina?

Ibn ´Uthaymiyn: Ni nini huko kulijipua kwa kujitoa muhanga?

Muulizaji: Mtu anajilipua katikati ya maadui…

Ibn ´Uthaymiyn: Mtu anajilipua na kufa?

Muulizaji: Ndio.

Ibn ´Uthaymiyn: Haya tumekwishayajibu. Tumesema kuwa ambaye anafanya hivo ameiua nafsi yake na kwamba ataadhibiwa kwa kile alichotumia kujiua nafsi yake Motoni kwa muda mrefu, kama ilivyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kitendo hicho ni haramu kwake kwa sababu Allaah amesema:

وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ

“Wala msiziue nafsi zenu.”[1]

Lakini watu hawa wajinga wenye kufanya mambo haya na huku wakidhani kuwa matendo haya yanawakurubisha mbele ya Allaah, basi nataraji kuwa hawatoadhibiwa adhabu hiyo. Lakini hata hivyo hawapati thawabu. Kwa sababu walichokifanya ni dhambi endapo watakusudia kufanya hivo. Lakini wana ufahamu mbovu masuala haya na hivyo wanasamehewa. Jengine ni kwamba sisi hatupelelezi nia, lakini kitendo hichi kweli kimefanywa kwa ajili ya Allaah ili neno Lake liweze kuwa juu au ni kwa ajili ya kulipa kisasi kwa ajili ya nafsi zao wenyewe? Hatujui. Allaah pekee ndiye anayejua. Pamoja na hivyo tunapaswa kupambanua kati ya yule anayepambana na adui kwa ajili ya kulipiza kisasi na yule anayepambana ili neno la Allaah liweze kuwa juu. Ni nani kati ya hao ambaye yuko katika njia ya Allaah? Ni yule anayepambana ili neno la Allaah liweze kuwa juu. Kuhusu ambaye anapambana kwa ajili ya kulipiza kisasi kutokana na watu waliomshambulia hawi mwenye kupigana katika njia ya Allaah. Kwa ajili hiyo tunapaswa tuwe wenye akili ili tusikose nusura. Ummah wa Kiislamu wenye mamilioni ya waislamu wamekosa nusura dhidi ya mayahudi, washirikina au wengieneo kwa sababu hawakupita ile njia inayotakikana. Kwanza wanatenda dhambi kwa wingi. Ni wenye kughafilika kwa wingi. Baadhi yao wanapambana na maadui lakini wao wenyewe hawaswali. Kwa hivyo ni lazima kwetu kupambana na nafsi zetu wenyewe na kurekebisha njia yetu ya kumwendea Allaah (´Azza wa Jall) kabla ya kujaribu kurekebisha njia za wengine.

Kwa kufupiza ni kwamba kujitoa muhanga ni jambo la haramu. Ambaye anafanya hivo ameiua nafsi yake mwenyewe na ameiweka nafsi yake katika adhabu kubwa yenye maana kwamba ataadhibiwa kwa kile alichotumia kuiua nafsi yake Motoni ambapo atakaa humo kwa muda mrefu. Lakini ambaye atafanya hivo kwa ujinga au ufahamu mbaya, basi nataraji kwa Allaah hatomwadhibu adhabu hii.

[1] 04:29

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftûh (125 B)
  • Imechapishwa: 25/12/2020